Posted By Posted On

CARLINHOS AMPA MKATABA MNONO LAMINE MORO YANGA

NA JESSCA NANGAWE UWEZO mkubwa wa kupiga krosi aliouonyesha kiungo mpya wa Yanga raia wa Angola, Carlos Fernandez Carlinhos, na jinsi beki wa timu hiyo, Lamine Moro, alivyoweza kuzipokea na kupachika mabao umemuwezesha Mghana huyo kuandaliwa mkataba mpya haraka. Kwasasa jina la Lamine Moro limeendelea kuteka vichwa vya mashabiki wa Yanga hususan baada ya kuhusika
The post CARLINHOS AMPA MKATABA MNONO LAMINE MORO YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA JESSCA NANGAWE

UWEZO mkubwa wa kupiga krosi aliouonyesha kiungo mpya wa Yanga raia wa Angola, Carlos Fernandez Carlinhos, na jinsi beki wa timu hiyo, Lamine Moro, alivyoweza kuzipokea na kupachika mabao umemuwezesha Mghana huyo kuandaliwa mkataba mpya haraka.

Kwasasa jina la Lamine Moro limeendelea kuteka vichwa vya mashabiki wa Yanga hususan baada ya kuhusika katika mabao mawili na kuifanya timu yake kuvuna alama 10 mpaka sasa.

Mabao hayo aliyopachika beki huyo, Carlinhos ndiye aliyempikia, kiasi cha kuonekama kuwa na uelewano zaidi wanapocheza pamoja uwanjani.

Ubora wa beki huyo kisiki wa Yanga umeendelea kumweka kwenye ramani nyingine baada ya mabosi wake kuanza mchakato wa kumwongezea mkataba mwingine haraka iwezekanavyo.

Mkataba wa mlinzi huyo upo kwenye hatua za mwisho kumalizika na tayari utaratibu wa kumwongezea umeanza kimya kimya baina yake na viongozi wa Yanga.

DIMBA Jumatano lina taarifa kwamba, uongozi ulivutiwa na kazi aliyoifanya hivyo, uliuchungulia mkataba wake baada ya kurejea jijini Dar wakitokea Moro na kuona ipo haja ya kumuongezea mwingine ili kumweka huru ndani ya kikosi chao.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, ameliambia DIMBA Jumatano kuwa suala la mkataba wa beki huyo lipo ndani ya uongozi na bado wanahitaji huduma yake, hivyo hakutakuwa na njia yoyote ya kutompa kandarasi mpya.

“Kwasasa bado anatambulika kuwa ana mkataba na sisi, sio yeye tu, wapo wengi lakini kutokana na umuhimu wake ndani ya kikosi kulingana na mahitaji ya mwalimu hatuna budi kumalizana naye mapema,” alisema Mwakalebela.

Lamine Moro aliisaidia timu yake kupata alama tatu katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar uliomalizika wikiendi iliyopita lakini pia ni Mghana huyo aliyefunga bao la pekee na lake la kwanza msimu huu dhidi ya Mbeya City.

Taarifa ambazo DIMBA Jumatano ilizipata jana jioni huku ikiambatana na picha, zilimuonyesha mjumbe wa kamati ya usajili, Yanga, Injinia Hersi Said, na beki Lamine Moro zikieleza tayari mchezaji huyo ameshamwaga wino kukipiga Yanga kwa miaka miwili zaidi.

The post CARLINHOS AMPA MKATABA MNONO LAMINE MORO YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *