Posted By Posted On

‘FIRST ELEVEN’ HII IMEBAMBA YANGA

NA EZEKIEL TENDWA SI unaikumbuka ile ‘First eleven’ ya Yanga iliyoisambaratisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro? Sasa unaambiwa kikosi kile kimejizolea sifa kemkem kila kona huku wengine wakidai kuna baadhi ya timu zitaweka mpira kwapani. Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa wiki, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililowekwa wavuni na beki
The post ‘FIRST ELEVEN’ HII IMEBAMBA YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA EZEKIEL TENDWA

SI unaikumbuka ile ‘First eleven’ ya Yanga iliyoisambaratisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro? Sasa unaambiwa kikosi kile kimejizolea sifa kemkem kila kona huku wengine wakidai kuna baadhi ya timu zitaweka mpira kwapani.
Katika mchezo huo uliochezwa mwishoni mwa wiki, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililowekwa wavuni na beki wa kati, Lamine Moro, kutokana na mpira wa kona uliochongwa na kiungo, Carlos Carlinhos.
Kikosi hicho hicho kiliundwa na Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Mukoko Tonombe, Michael Sarpong, Carlos Carlinhos na Tuisila Kisinda.
Baadaye yalifanyika mabadiliko ambapo walitoka Sarpong, Carlinhos pamoja na Kisinda na nafasi zao kuchukuliwa na Ditram Nchimbi, Yacouba Sogne na Haruna Niyonzima ambapo wote waliuwasha moto vilivyo.
Kikosi hicho kilicheza vizuri na kuwafanya mashabiki wa Yanga waliohudhuria uwanjani kushangilia muda wote na kuiona timu yao kwamba inaweza kutwaa ubingwa msimu huu kwa kuwazidi kete watani zao wa jadi Simba.
Mpaka sasa Yanga wameshinda michezo mitatu kati ya minne waliyocheza wakishika nafasi ya tatu kwenye msimamo kwa pointi 10 sawa na Simba, zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam FC ndio wanaoongoza wakiwa na pointi 12 wakishinda michezo yao yote minne.
Mashabiki wa kikosi hicho wanajiandaa kupata burudani nyingine Jumamosi ya wiki hii Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo timu yao itapambana na Coastal Union ya jijini Tanga mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa.

The post ‘FIRST ELEVEN’ HII IMEBAMBA YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *