Posted By Posted On

NYOTA MTIBWA SUGAR ASHINDWA KUJIZUIA ASIFIA UWEZO WA SARPONG YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Winga wa Mtibwa Sugar, Haruna Chanongo amesema kiwango alichokion yesha straika wa Yanga, Michael Sarpong katika mechi yao, waliopigwa bao 1-0 ni tishio.

Chanongo alisema licha ya Sarpong kutokufunga bao katika mchezo huo, ndiye alikuwa mwiba kwa mabeki wao kutumia muda mwingi kumzibia mianya ya kuwadhuru, ndipo Lamine Moro alipata upenyo wa kuwaumiza.

“Ni mchezaji hatari, jamaa ni mpambanaji na analazimisha mashambulizi, akiendelea hivyo ataisaidia timu yake kufunga mabao mengi na atakuwa chachu kwa wazawa kwani lazima mchezaji wa kigeni awe na kitu cha tofauti na wenyeji wake,” alisema Chanongo na kuongeza.

“Ni kweli hakufunga lakini niliona namna ambavyo alikuwa anafanya mabeki wetu muda mwingi wawe wanamkaba ndio maana Moro alijiongeza na kufunga, ingawa ulikuwa mchezo mgumu na tulicheza kwa nidhamu ya hali ya juu,” alisema

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *