Posted By Posted On

SIMBA KUONGEZA MASHABIKI 60,000

NA MWANDISHI WETU SIMBA imeweka mkakati wa kuhakiki wanachama wake na kuongeza mashabiki zaidi ya 60,000 nchini katika kipindi kifupi kufikia Desemba mwaka huu. Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki wa Simba, Hamisi Kisiwa, akikabidhi kadi za mashabiki kwenye tawi la Ngurumo za Radi, Ukonga Mazizini jana, alisema ili Simba iwe ya kimataifa zaidi ni lazima
The post SIMBA KUONGEZA MASHABIKI 60,000 appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA MWANDISHI WETU

SIMBA imeweka mkakati wa kuhakiki wanachama wake na kuongeza mashabiki zaidi ya 60,000 nchini katika kipindi kifupi kufikia Desemba mwaka huu.

Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki wa Simba, Hamisi Kisiwa, akikabidhi kadi za mashabiki kwenye tawi la Ngurumo za Radi, Ukonga Mazizini jana, alisema ili Simba iwe ya kimataifa zaidi ni lazima iwe na mshabiki wengi kila kona ya Tanzania na nje ya nchi.

Alisema kadi za mashabiki zinatolewa kupitia matawi ya Simba kwa kujisajili na kulipa fedha benki ya Equity ambayo imeingia mkataba na klabu hiyo.

Kisiwa ambaye amekabidhiwa wadhifa huo hivi karibuni alisema wanachama wa Simba muda si mrefu wataingizwa kwenye hisa.

Alisema kampeni ya kuingiza mashabiki nchi nzima imeshika kasi na tayari mikoa mbalimbali imejiandikisha na kuomba kukabidhiwa kadi za mashabiki.

Ofisa Habari na Masoko wa Simba, Jacob Gamaly, alisema sambamba na kutoa kadi za mashabiki pia kila mkoa umeandaa sherehe za kupokea kombe la ubingwa msimu 2019/20.

Mkuu wa Hamasa na burudani wa tawi la Ngurumo za Radi, Lameck Mwalimu, alisema tawi hilo lina mipango ya kununua basi ambalo litawapeleka wanachama wao kila Simba itakapocheza nchini.

Mashabiki na wapenzi wa Simba wa tawi hilo na matawi ya jirani ya Kitunda, Ukonga, Chanika na Uwanja wa Ndege waliohudhuria hafla hiyo wameahidi kufika uwanjani kwa wingi kila timu yao itakapokuwa inacheza.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga, Jerry Slaa, akitoa salamu kwa mashabiki wa Simba alisema yeye ni mshabiki wa Yanga na anatamani sana siku moja klabu yao ifuate nyayo za watani zao kwa maendeleo.

The post SIMBA KUONGEZA MASHABIKI 60,000 appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *