Posted By Posted On

YANGA KILA MECHI NI KAMA FAINALI

NA EZEKIEL TENDWA BAADA ya kupata ushindi katika michezo yao mitatu kati ya minne waliyokwishacheza mpaka sasa Ligi Kuu Tanzania Bara, mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo, Yanga, wametamba kwamba kila timu itakayowasogelea haitatoka salama. Katika misimu mitatu mfululizo iliyopita, ubingwa wa Ligi Kuu Bara umekuwa ukichukuliwa na Simba kitu ambacho kimewaudhi sana Yanga ambao
The post YANGA KILA MECHI NI KAMA FAINALI appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA EZEKIEL TENDWA

BAADA ya kupata ushindi katika michezo yao mitatu kati ya minne waliyokwishacheza mpaka sasa Ligi Kuu Tanzania Bara, mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo, Yanga, wametamba kwamba kila timu itakayowasogelea haitatoka salama.

Katika misimu mitatu mfululizo iliyopita, ubingwa wa Ligi Kuu Bara umekuwa ukichukuliwa na Simba kitu ambacho kimewaudhi sana Yanga ambao wamesema, msimu huu iwe mvua au jua, lazima kieleweke.

Kudhihirisha kwamba wamedhamiria kufanya kweli msimu huu, Wanajangwani hao wamefanikiwa kukusanya pointi sita katika michezo miwili migumu waliyocheza ugenini wakianza dhidi ya Kagera Sugar, mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na kushinda bao 1-0 kabla ya kufanya hivyo tena dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Baada ya michezo hiyo miwili ugenini, sasa mabingwa hao wanarudi Uwanja wa Mkapa kuwakabili Coastal Union, Jumamosi wiki hii, ambapo kocha mkuu wa kikosi hicho, Zlatko Krmpotic, amewaambia wachezaji wake anataka kuona wakishinda idadi kubwa ya mabao.

Katika michezo yote mitatu ambayo Yanga wameshinda, wamekuwa wakifunga mabao yasiyozidi mawili kitu ambacho kimemfanya kocha huyo kuifanyia kazi safu yake ya ushambuliaji, kuhakikisha kila timu itakayowasogelea inaoga mabao ya kutosha.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, kocha huyo alisema kwasasa anaendelea kuwasuka vijana wake kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union na michezo mingine ijayo ili kuhakikisha msimu huu wanatimiza malengo yao ya kutwaa ubingwa.

“Ligi kwa ujumla ni ngumu lakini ninaamini kwamba kadri muda unavyokwenda kikosi changu kinazidi kuimarika na tutapata ushindi mkubwa. Kikubwa kwetu ni pointi tatu,” alisema.

Kocha huyo anajivunia kuwa na wachezaji mahiri waliosajiliwa msimu huu akiwamo Tuisila Kisinda, Tonombe Mukoko, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ na wengine ambao wamekuwa chachu ya ushindi kwa Wanajangwani hao.

Katika michezo miwili ya hivi karibuni, Carlinhos amekuwa gumzo kutokana na ufundi wake wa kupiga mipira iliyokufa ambayo ilizaa matunda na Yanga kuibuka na pointi zote tatu muhimu akianza dhidi ya Mbeya City ambapo alichonga kona ikatua kwenye kichwa cha Lamine Moro na kuujaza wavuni na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, hali ilikuwa hivyo hivyo ambapo Muangola huyo alipiga kona ambayo iliunganishwa vizuri na Lamine Moro kwa guu lake la kulia na kujaa wavuni na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

The post YANGA KILA MECHI NI KAMA FAINALI appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *