Posted By Posted On

ZLATKO:HAKUNA MDA WA KUPOTEZA YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Licha ya kikosi chake kutoa ‘dozi’ katika mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa Yanga, Zlakto Krmpotic, amesema mkakati wake kwa sasa ni kupata michezo ya kirafiki zaidi, ili timu yake icheze kwa kuzoeana na kupata muunganiko bora na hatimaye kutimiza malengo .

 

Akizungumza na chanzp chetu hapo jana, Zlatko alisema licha ya kushinda katika mechi zao tatu za ligi, wachezaji wake wameonyesha kupambana na kutokuwa na muunganiko mzuri kwa sababu ya kukosa matayarisho ya kuanza kwa ligi hiyo.

Zlatko alisema licha ya kuhitaji muda na kutumia mechi za ligi kutafuta matokeo pamoja na kupata muunganiko, pia mechi za kirafiki wanazocheza zinasaidia wachezaji wake kupata uzoefu na muunganiko mzuri.

“Sasa hivi hatuna muda wa kupoteza, tunatumia mechi za ligi kutafuta matokeo chanya, lakini kujenga kombinesheni kwa wachezaji wangu, pia kutumia muda huu kupata mechi za kirafiki ambazo nazo zitanisaidia kupata kile ninachokitarajia ndani ya kikosi changu,” alisema Zlatko.

Alisema kulingana na mapungufu ambayo amekuwa akiyaona katika kikosi chake, kubwa ni suala la muunganiko jambo ambalo analifanyia kazi kwa kupata mechi za kirafiki pamoja na kwenye ligi hiyo.

“Suala la ushambuliaji nalo bado hii inatokana na timu hiyo kutopata muda wa kukaa pamoja, haijalishi tunashinda bao 1-0 kila mechi kikubwa ni kupambana kutafuta pointi tatu zitakazotuweka katika nafasi nzuri na kufikia malengo yetu,” alisema Zlatko.

 

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *