Posted By Posted On

ALICHOSEMA KOCHA MSAIDIZI YANGA BAADA MECHI YA KIRAFIKI DHIDI KMKM

Msomaji wa Yanganews Blog:Benchi la ufundi la Yanga lina matumaini makubwa ya kuendelea kufanya vizuri kwenye michezo ya Ligi Kuu, baada ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM kutoka visiwani Zanzibar jana Jumatano, jijini Dar es salaam.

Yanga waliutumia mchezo huo uliomalizika kwa ushindi wa mabao mawili kwa sifuri, kama sehemu ya kujiandaa na mchezo wa mzunguuko watano wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam, Jumamosi Oktoba 03.

Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema kuwa wanaamini kwa maandalizi ambayo wanayafanya, watapata matokeo chanya kwenye michezo ijayo ya Ligi Kuu, wakianza na mchezo dhidi ya Coastal Union.

Amesema kuwa ana imani kwamba wachezaji wake watakuwa kwenye ubora kwa kadri ambavyo wanaendelea kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja, pamoja na kucheza kwa kujituma.

“Sio kazi nyepesi kupata ushindi ndani ya uwanja, ila inahitaji maandalizi mazuri na makubwa. Tunachokifanya kwa sasa ni kuona tunakuwa na timu bora itakayotupa matokeo hivyo tutapambana mbele ya Coastal Union kupata ushindi.

“Timu nzuri ambayo tunakutana nayo hatuibezi tunawaheshimu wapinzani wetu lakini hamna namna tunahitaji ushindi na kupata pointi tatu, mashabiki wajitokeze kwa wingi,” amesema kocha huyo ambaye aliwahi kuinoa Mbyea City ya Mbeya.

Kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, mabao ya Yanga yalifungwa na kiungo kutoka DR Congo Mukoko Tonombe dakika ya 10 na 30.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *