Posted By Posted On

DONDOO ZA MKUTANO WA YANGA NA WANAHABARI – Uongozi wa klabu ya Yanga umesema mkataba wa Bernard Morrison na Simba unamapungufu…

DONDOO ZA MKUTANO WA YANGA NA WANAHABARI

– Uongozi wa klabu ya Yanga umesema mkataba wa Bernard Morrison na Simba unamapungufu makubwa, viongozi wa Simba hakuna sehemu waliyosaini kwa mujibu wa FIFA kwenye mkataba huo.

– Kutokana na mapungufu hayo FIFA imekataa kuungiza mkataba huo kwenye system hivyo FIFA wanamtambua Bernard Morrison kuwa ni mchezaji wa Yanga.

– Pia wametoa document ya uthibitisho kuwa Yanga wameenda kwenye Mahakama ya usuluhishi Michezoni Duniani (CAS)

– Wameendelea kusema, mpaka sasa FIFA inatambua kuwa Bernard Morrison ni mchezaji halali wa Yanga na bado hawaja cancel mkataba wake na Yanga.

– Wamesema mkataba huo wa Simba ambao unamapungufu wameupeleka CAS kama ushahidi na uthibitisho.

– TFF inatakiwa iwanyang’anye point zote katika mechi walizocheza Simba kwa sababu mkataba wa Morrison na Simba uko kimakosa na FIFA inamtambua kuwa ni mchezaji wa Yanga.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *