Posted By Posted On

KOCHA MKUU AMKOMALIA SARPONG YANGA

Msomaji wa Yanganews Blog:Mshambuliaji wa Yanga, Michael Sarpong ametakiwa kutuliza akili na kuangalia mikimbio yake upya kwa ajili ya kuifungia miamba hiyo ya soka nchini.

Kocha wa Yanga, Zlatko Krmpotic alimtumia Sarpong katika mchezo wa juzi wa kirafiki dhidi ya KMKM uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, lakini hakufanikiwa kufunga licha ya kucheza kwa deakika 45 za kipindi cha pili.

Baada ya mchezo huo wa juzi usiku, Krmpotic alisema Sarpong anatakiwa kutuliza akili, kuweka akili uwanjani na kukaa katika maeneo ya kufunga.

Kocha huyo raia wa Serbia alisema mshambuliaji huyo ana uwezo mkubwa wa kucheza katika nafasi yake, lakini anatakiwa kuelekeza akili katika kufumania nyavu, suala ambalo ameshazungumza naye.

“Ni mchezaji mzuri na mwenye kila kitu cha mshambuliaji, suala la kutokuwa na mabao mengi hata mimi silifurahii kutokana na kutomaliza mechi mapema.

“Unapofunga mabao mengi unaimaliza mechi mapema, na suala la Sarpong nadhani ni la muda kidogo, anatakiwa kufikiria tu zaidi uwanjani na kuachana na gharama za usajili, kwasasabu anajua klabu na mashabiki.

“Naamini atabadilika na kuwa bora zaidi, tumezungumza na anajua sasa nini cha kufanya, kuanzia kwenye kukaa katika nafasi na mikimbio yake uwanjani kutoa nafasi,” alisema.

 

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *