Posted By Posted On

Photos from VIWANJANI LEO’s post

BODI YA LIGI YASHUSHA RUNGU KWA TIMU KADHAA IKIWEMO YANGA

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imezipiga faini na kuzionya timu kadhaa za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa makosa tofautitofauti ikiwemo ukiukwaji wa kanuni za Ligi Kuu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Bodi hiyo, Yanga SC, imepigwa faini ya Shilingi 500,000 (laki tano) kwa kosa la mashabiki wake kuwafanyia vurugu mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Simba kwenye mchezo kati yake na Mtibwa Sugar, uliopigwa Septemba 27, Morogoro.

Yanga Pia imepigwa faini ya Shilingi 500,000 (laki tano) kwa kosa la mashabiki wake kusukuma geti kwa nguvu na kuingia sehemu ya kuchezea (pitch) kwa wingi na kusababisha mahojiano yaliyokuwa yakifanywa na Azam TV na manahodha kukatishwa na kushindikana kuendelea.

Timu zingine zilizokumbwa na adhabu ya faini ni pamoja na Kagera Sugar, Mbeya City na KMC ambayo pia imepewa onyo kali.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *