Posted By Posted On

YANGA YALIANZISHA UPYAA, SAKATA LA MORRISON

Msomaji wa Yanganews Blog:Klabu ya Yanga SC kupitia makamu mwenyekiti Fredrick Mwakalebela leo amesema kuwa mchezaji Bernard Morrison kwenye mfumo wa FIFA wa usajili Morrison bado anasomeka kuwa ni mchezaji wao Yanga.

Mwakalebela anasema mkataba wa Simba na Morrison una mapungufu sababu hauna saini ya kiongozi wa Simba zaidi ya Morrison mwenyewe hivyo Morrison bado ni mchezaji wao.

“Kwa maana hiyo mkataba wa Morrison ukiangalia kwa karibu kwa jicho la kisheria na mtu wa kawaida unaonekana kuwa umesainiwa na upande mmoja, kwa maana hiyo inaonesha kuwa Simba SC ya Dar es Salaam haijaridhia mkataba wa Morrison kwa sababu hakuna sehemu yoyote ambapo club ya Simba imesaini mkataba”Mwakalebela

Kama utakuwa unakumbuka vizuri kamati ya sheria na hadhi za Wachezaji ya TFF baada ya Morrison kukana kuwa na mkataba na Yanga, walipitia na kujiridhisha kuwa mchezaji huyo ni huru ikiwa ni siku chache zimepita akiwa ametoka kutangazwa kusaini Simba SC.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *