Posted By Posted On

YANGA YAENDELEZA KUANDAMWA TFF, YAPIGWA FAINI MILIONI MOJA

Msomaji wa Yanganews Blog:Mashabiki wawili wa Yanga wanaofahamika kwa majina maarufu ya Osama na Jesca wamefungiwa kuingia uwanjani kwa kipindi cha miezi 12, kwa kosa , wametajwa kushiriki tukio la kuwapiga na kuwachania jezi mashabiki waliokuwa wamevaa jezi za Simba.

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ambayo iliwapa adhabu mashabiki hao pia katika kikao chake cha Septemba 30, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye ligi.

Wakati mashabiki wao wakifungiwa kuingia uwanjani, klabu ya Yanga imetozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la mashabiki wa timu hiyo waliokuwa upande wa Kaskazini kusukuma geti kwa nguvu na kuingia eneo la kuchezea (pitch) kwa wingi jambo lililopelekea mahojiano kati ya Azam TV na manahodha kukatishwa na kushindikana kuendelea katika mchezo uliochezwa Septemba 27, 2020 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Yanga wamepewa adhabu hiyo kwa uzingativu wa kanuni ya 45:1 ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa klabu huku wakipigwa tena faini ya Sh. 500,000  kwa kosa la mashabiki wa timu yake kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa kuwapiga na kuwachania jezi mashabiki wanaohisiwa ni wa Simba waliovaa jezi za Simba katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja huo.

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *