Posted By Posted On

MANCHESTER UNITED YACHAPWA 6-1 NA TOTTENHAM HOTSPUR OLD TRAFFORD

TIMU ya Tottenham Hotspur imeitandika Manchester United mabao 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford. 
Manchester United inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Mnorway Ole Gunnar Solskjaer waliwachokoza Spurs kwa bao la Bruno Fernandes kwa penalti dakika ya pili tu.   
Spurs ikazinduka kwa mabao ya Tanguy Ndombele dakika ya nne, Heung-min Son mawili dakika ya saba na 37, Harry Kane dakika ya 30 na 79 kwa penalti na Serge Aurier dakika ya 51.


Wachezaji wa Tottenham Hotspur wakishangilia ushindi wao wa 6-1 dhidi ya Manchester United leo Uwanja wa Old Trafford PICHA ZAIDI GONGA HAPA

 

Manchester United ilimaliza pungufu baada ya Anthony Martial kutolewa kwa kadi nyekundu kumchezea vibaya Erik Lamela wakati wakigombea mpira kwenye kona.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *