Posted By Posted On

MASHABIKI YANGA WAMPA TUZO MUKOKO TONOMBE

Msomaji wa Yanganews Blog:Kiungo Mukoko Tonombe amechaguliwa na mashabiki wetu kuwa mchezaji bora wa Mwezi Septemba wa kikosi cha Yanga.

Mukoko ameshinda kwa 40% ya kura 2079 zilizopigwa na mashabiki walioshiriki zoezi hilo kupitia ukurasa wa Mtandao wa Twitter wa @yangasc1935.

Mchuano wa kuwania mchezaji Bora ulihusisha wachezaji wanne wote wa Kimataifa ambao walishinda tuzo za mchezaji bora wa mechi kutokana na kura za mashabiki.

Mratibu wa Tuzo hiyo, Hassan Bumbuli amewashukuru mashabiki wa Yanga kuwa namna ambavyo wamelipokea wazo hilo na kushiriki kwa wingi.

“Tunawashukuru sana Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kuwa kufanikisha zoezi hili, ndio kwanza tumeanza na tunaamini tutakwenda vizuri msimu mzima,” amesema.

Wachezaji wengine walioingia kwenye tuzo ya mwezi ni beki kisiki Lamine Moro aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata 31%, Carlos Carlinhos 21% na Mshambuliaji Michael Sarpong, aliyepata 8%

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *