Posted By Posted On

Coutinho kufanya makubwa Barcelona

CATALUNYA, Hispania

KIUNGO wa Barcelona, Philippe Coutinho, ameinusuru timu yake kukumbana na kichapo kutoka kwa Sevilla baada ya kufunga bao la kusawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Baada ya kufunga bao hilo, Coutinho ambaye alikuwa akikipiga kwa mkopo msimu uliopita ndani ya kikosi cha Bayern Munich, alidokeza kutaka nafasi zaidi ndani ya Camp Nou anaamini atafanya vizuri akiwa hapo.

“Nahitaji kufanikiwa nikiwa na kikosi hiki, nina njaa na kufanya kazi kwa juhudi ili kuhakikisha napata nafasi ya kuwepo hapa kwa muda mrefu zaidi,” alisema.

Mpaka sasa katika michezo mitatu aliyocheza, mchezaji huyo raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 28, amefunga bao moja na kutoa asisti mbili.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *