Kumbe Aouar ndo kaikataa Arsenal
PARIS, Ufaransa
KIUNGO wa Lyon, Houssem Aouar, amevunja ukimya na kusema hakuona sababu ya kuondoka ndani ya kikosi hicho cha Ufaransa na kukimbilia Arsenal ambao walimuhitaji kwa udi na uvumba.
Aouar amekuwa akihusishwa kutakiwa vikali na Arsenal ambao walikuwa tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 30 pamoja na Matteo Guendouzi.
Hata hivyo, kiungo huyo ameamua kubaki nchini Ufaransa kuendelea kuwatumia Lyon na kuzima tetesi za kutaka kujiunga na Arsenal inayofundishwa na Mikel Arteta.
“Naamini naweza kuendelea kutoa kitu hapa, nahitaji kuendelea kuwa katika timu ambayo nimeanza nayo maisha ya soka kwa muda mrefu zaidi,” alisema.
,
Comments (0)