Posted By Posted On

Mourinho: Tusiwacheke Man United jamani

LONDON, England

KOCHA wa Tottenham, Jose Mourinho amewataka mashabiki wa soka waache kuwacheka Manchester United ambao walikubali kichapo cha mabao 6-1, katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford.

Mourinho aliyewahi kuifundisha Manchester United, kabla ya kufukuzwa Desemba mwaka 2018, alisema hayo mara baada ya kikosi chake cha Tottenham kuwachakaza wapinzani wao.

“Ni ngumu kuja hapa na kupata ushindi huu, lakini, hawa ni Manchester United, tusisahau wanaweza kurudi na kuwa imara zaidi baada ya kufungwa sababu wao ni Manchester United.

“Nimesikia wamemsajili Edinson Cavani na beki mwngine, siunaona jinsi walivyojipanga kurudi katika ubora wao, lazima uwe na wachezaji wenye uwezo wa kufanya hivyo,” alisema.

Tanguy Ndombele, Son Hueng-Min (2), Harry Kane (2) na Serge Aurier walifunga mabao kwa upande wa Tottenham huku Bruno Fernandes akifanya hivyo kwa Manchester United.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *