Posted By Posted On

TUNATEKELEZA KUWA KARIBU NA WANANCHI-MSOLLA

Msomaji wa Yanganews Blog:Dkt. Msolla ameyasema hayo alipokutana na Wanachama na Wapenzi wa Yanga katika Tawi la Nzega mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya ziara yake kutembelea matawi kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi.

โ€œTuliahidi kuwa karibu na wenye Timu ambao ndio Wanachama na Wapenzi hivyo ushiriki wenu wa moja kwa moja ni pamoja na kutoa maoni juu ya masuala yanayoihusu Klabu na timu yenu, sisi tunapokea maoni na yanafanyiwa kazi,โ€ amesema Dkt. Msolla.

Aidha Mwenyekiti amewaeleza Wanachana na Wapenzi wa Yanga juu ya umuhimu wa ushiriki wao katika kujenga Yanga ambayo itajitegemea mtaji ukiwa ni wingi wa wanachama na wapenzi.

โ€œIli tuweze kujitegemea ni lazima tuwe na mtaji mkubwa wa Wanachama an Wapenzi, hivyo Wanachama na Wapenzi wanapatikana kwenye Matawi kwa hiyo matawi ni nguzo muhimu katika kujenga maendeleo endelevu ya Klabu yetuโ€ amesema.

Katika ziara hiyo, Mwenyekiti Dkt. Msolla alitembelea matawi katika maeneo ya Singida, Igunga, Kahama, Geita, Sengerema, Mwanza na Bariadi.

ย 

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *