Posted By Posted On

Atletico: Arsenal wahuni sana jamani

MADRID, Hispania DIEGO Simeone hajafurahishwa na Arsenal jinsi ilivyomnasa kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey, ikiwa zimebaki dakika 32 kabla ya dirisha la usajili kufungwa juzi usiku. Partey alikuwa katika mipango ya msimu huu ya Simeone, lakini, ilikuwa ngumu kuendelea kuwa naye kwani Arsenal waliweka dau ambalo lilimruhusu kuondoka ndani ya Wanda Metropolitano. Kocha huyo
The post Atletico: Arsenal wahuni sana jamani appeared first on Gazeti la Dimba.,

MADRID, Hispania

DIEGO Simeone hajafurahishwa na Arsenal jinsi ilivyomnasa kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Partey, ikiwa zimebaki dakika 32 kabla ya dirisha la usajili kufungwa juzi usiku.

Partey alikuwa katika mipango ya msimu huu ya Simeone, lakini, ilikuwa ngumu kuendelea kuwa naye kwani Arsenal waliweka dau ambalo lilimruhusu kuondoka ndani ya Wanda Metropolitano.

Kocha huyo raia wa Argentina aliamini nyota huyo wa Ghana angesalia Madrid, sababu alikuwa akiwasiliana naye mambo mbalimbali yaliyohusu mbinu na ufundi wa Atletico Madrid.

Klabu hiyo ya Hispania wanatajwa kukasirika na jinsi Arsenal ilivyofanya usajili hilo bila kuwasiliana nao juu ya Partey.

Washika Bunduki hawakuwasiliana na Atletico kama watalipa kiasi cha pauni milioni 45 ambacho kinamruhusu Partey kuondoka.

“Shirikisho la Soka Hispania, La Liga, waliwasiliana nasi zikiwa zimesalia dakika 32 dirisha la usajili kufungwa kuwa Arsenal wamelipa kiasi kilichopo kwenye mkataba wa Thomas, hatujafurahishwa na jinsi jambo lilivyoenda,” ilisema taarifa ya Atletico.

Inaaminika kiungo huyo raia wa Ghana atalipwa kiasi cha pauni 250,000 kwa wiki na ongezeko la pauni milioni 1.8 kitaongezwa baadae.

Partey amesaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia Arsenal huku kukiwa na makubaliano ya kuongeza mwaka. Thomas aliitumikia Atletico katika michezo 188 kwa kipindi cha miaka mitano.

The post Atletico: Arsenal wahuni sana jamani appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *