Posted By Posted On

Dah! Shaqiri akutwa na corona

MERSEYSIDE, England XHERDAN Shaqiri anakuwa mchezaji wa tatu wa Liverpool kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona ndani ya wiki, kwani, ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa England wapo Thiago Alcantara na Sadio Mane. Sasa, Shaqiri mwenye umri wa miaka 28 amekutwa na virusi vya corona baada ya kupimwa akiwa katika majukumu ya timu
The post Dah! Shaqiri akutwa na corona appeared first on Gazeti la Dimba.,

MERSEYSIDE, England

XHERDAN Shaqiri anakuwa mchezaji wa tatu wa Liverpool kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona ndani ya wiki, kwani, ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa England wapo Thiago Alcantara na Sadio Mane.

Sasa, Shaqiri mwenye umri wa miaka 28 amekutwa na virusi vya corona baada ya kupimwa akiwa katika majukumu ya timu ya Taifa ya Switzerland.

Taarifa hiyo ilithibitishwa na Chama cha Soka cha Switzerland, itakumbukwa wiki imepita tangu Alcantara alipokutwa na maambukizi hayo kabla ya Mane.

Tangu ajiunge na Liverpool kutoka Bayern Munich, kiungo huyo raia wa Hispania alicheza mchezo mmoja dhidi ya Chelsea ambao aliingia kipindi cha pili.

Hata hivyo, alikosa mchezo wa Kombe la Ligi, Arsenal na ule ambao Liverpool walichapwa mabao 7-2 dhidi ya Aston Villa ndani ya Uwanja wa Villa Park.

The post Dah! Shaqiri akutwa na corona appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *