Posted By Posted On

Eeh! Man United wampigia simu Pochettino

MANCHESTER, England TAARIFA kutoka katika vyanzo mbalimbali Ulaya vinasema mabosi wa Manchester United wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino. Manchester United walikubali kichapo cha mabao 6-1 kutoka kwa Tottenham na kufanya mabosi hao kuwa na maswali mengi juu ya mwenendo wa kikosi chao tangu kuanza kwa msimu huu chini ya Ole
The post Eeh! Man United wampigia simu Pochettino appeared first on Gazeti la Dimba.,

MANCHESTER, England

TAARIFA kutoka katika vyanzo mbalimbali Ulaya vinasema mabosi wa Manchester United wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino.

Manchester United walikubali kichapo cha mabao 6-1 kutoka kwa Tottenham na kufanya mabosi hao kuwa na maswali mengi juu ya mwenendo wa kikosi chao tangu kuanza kwa msimu huu chini ya Ole Gunnar Solskjaer.

Kocha huyo raia wa Norway alishuhudia kikosi chake kikimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita huku wakiishia hatua ya nusu fainali kwenye Ligi ya Europa.

Lakini, tangu kuanza kwa msimu huu anaonekana kushindwa kufanya vizuri, Manchester United imeruhusu kufungwa mabao 11 katika michezo mitatu ya Ligi Kuu.

Kutokana na kiwango hicho, inaelezwa Ed Woodward alifanya mawasiliano na Pochettino ikielezwa amemwambia akae mkao wa kula, kwani Solskjaer anaweza kuondolewa wakati wowote kaa timu hiyo itaendelea kufanya vibaya.

Pochettino ambaye aliiongoza Tottenham katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2019, alitimuliwa Novemba mwaka jana na alikuwa akihusishwa kutakiwa na klabu mbalimbali kubwa Ulaya.

The post Eeh! Man United wampigia simu Pochettino appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *