Posted By Posted On

FOWADI SIMBA WEMBE, YANGA UKUTA CHUMA

NA EZEKIEL WAKATI mashabiki wa soka nchini wakiusubiria kwa hamu kubwa mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga, rekodi za timu hizo katika michezo mitano waliyokwisha kucheza mpaka sasa inaufanya mchezo huo kutabiriwa kuwa mgumu sana. Katika michezo hiyo, kila timu inayo rekodi yake ya kusisimua na kuufanya mchezo huo kuvuta hisia za mashabiki
The post FOWADI SIMBA WEMBE, YANGA UKUTA CHUMA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA EZEKIEL WAKATI mashabiki wa soka nchini wakiusubiria kwa hamu kubwa mtanange wa watani wa jadi Simba na Yanga, rekodi za timu hizo katika michezo mitano waliyokwisha kucheza mpaka sasa inaufanya mchezo huo kutabiriwa kuwa mgumu sana.

Katika michezo hiyo, kila timu inayo rekodi yake ya kusisimua na kuufanya mchezo huo kuvuta hisia za mashabiki wengi ndani na nje ya nchi.

Mpaka sasa, timu zote 18 zinazoshiriki ligi hiyo zimeshacheza michezo mitano kila moja huku Yanga wakishikilia rekodi ya kufungwa mabao machache kuliko timu yoyote ile na Simba wakiendeleza rekodi yao ya kufunga mabao mengi.

Yanga wamefungwa bao moja tu katika michezo hiyo mitano, bao ambalo lilipatikana katika mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

Baada ya hapo, safu hiyo ya ulinzi ya Yanga chini ya Lamine Moro na Bakari Mwamnyeto, haikutaka kuruhusu tena nyavu zao kuchezewa na badala yake wao ndio wakawa wanatembeza vichapo.

Mbali na kutokuruhusu mabao mengine, safu ya ulinzi ya Yanga imekuwa chachu kubwa katikia kuipatia timu pointi tatu muhimu kwani Moro anaongoza akiwa na mabao mawili.

Moro ambaye mara kwa mara ndiye anayevaa kitambaa cha unahodha, aliipa Yanga pointi tatu muhimu akifunga bao katika ushindi wa 1-0 Uwanja wa Mkapa dhidi ya Mbeya City, huku akifanya hivyo tena mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Beki huyo ambaye hivi karibuni ameongeza mkataba wa miaka miwili ndiye anayeongoza Yanga akiwa na mabao mengi huku akifuatiwa na Michael Sarpong aliyefunga bao dhidi ya Prisons mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Wengine wenye bao moja ni Tonombe Mukoko aliyefunga dhidi ya Kagera Sugar wakati Yanga wakipata ushindi wa bao 1-1, Carlos Carlinhos, Haruna Niyonzima na Yacouba Sogne, katika mechi ambayo Yanga iliifunga Coastal Union mabao 3-0.

Kwa upande wa Simba, safu yao ya ushambuliaji inaonekana kuzidi kuwa wembe hatari kwani wanaongoza kwa kupachika jumla ya mabao 14 wakifuatiwa na Azam FC wenye mabao tisa, KMC mabao nane na Yanga mabao saba.

Mabao hayo ya Simba yamefungwa na Meddie Kagere mwenye manne, Chris Mugalu mabao matatu, Mzamiru Yassin pamoja na Clatous Chama mawili kila moja, huku John Bocco, Pascal Wawa na Luis Miquissone wakiwa na bao moja kila mmoja.

Jambo la kufurahisha kuelekea katika mtanange huo wa Oktoba 18 ni kwamba timu hizo zimelingana pointi, kila moja ikiwa na alama 13 zikipishana mabao ya kufunga na kufungwa.

Azam FC ndio ambao wapo kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 15 katika michezo yao mitano waliyokwisha kucheza wakiweka rekodi ya kushinda yote wakifunga mabao tisa na kufungwa mabao mawili.

Kuelekea Oktoba 18 swali ni je safu ya ushambuliaji ya Simba itaendeleza makali yake ya kupachika mabao au itakwama mbele ya ukuta wa chuma wa Yanga?

Tayari homa ya pambano hilo imeshaanza kupanda kila kona kwa mashabiki wa timu hizo kurushiana vijembe kupitia mitandao ya kijamii kila mmoja akisifu upana wa kikosi chake na kujinasibu atashinda mchezo huo.

The post FOWADI SIMBA WEMBE, YANGA UKUTA CHUMA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *