Posted By Posted On

JOEL LWAGA Mkali wa Injili anayemzimia Diamond Platinum

NA GLORY MLAY UKIACHILIA mbali ushindani uliopo katika muziki wa bongo fleva, pia katika injili mambo pia ni moto.Sio kazi kazi rahisi kutoka hukupambana kufa na kupona. Katika muziki wa Injili hapa nchini wapo wasanii wanaokuja kwa kasi na kulitawala soko la muziki huo.Miongoni mwa orodha hiyo wapo wasanii Joel Lwaga, Goodluck Gozbert, Ambwene Mwasongwe,
The post JOEL LWAGA Mkali wa Injili anayemzimia Diamond Platinum appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA GLORY MLAY
UKIACHILIA mbali ushindani uliopo katika muziki wa bongo fleva, pia katika injili mambo pia ni moto.Sio kazi kazi rahisi kutoka hukupambana kufa na kupona.
Katika muziki wa Injili hapa nchini wapo wasanii wanaokuja kwa kasi na kulitawala soko la muziki huo.Miongoni mwa orodha hiyo wapo wasanii Joel Lwaga, Goodluck Gozbert, Ambwene Mwasongwe, Paul Clement, Walter Chilambo na Angel Benard, Christina Shusho na wingineo wengi.
Leo katika uwanja huu tunaye Joel Lwaga mwanamuziki ambaye anwika nyimbo zake kama
Lwaga amefanikiwa kukonga nyoyo za watu na nyimbo mbalimbali kama ‘Sitabaki Kama Nilivyo’, Wew ni Wajuu, Watanitazama, ‘Yote Mema’ na nyinginezo nyingi.
DIMBA Jumatano limefanya mahojiano na Lwaga ili kufahamu maisha yake nje ya muziki wa kiroho anoufanya.
DIMBA: Je katika maisha yako ulishawahi kutongozwa na wanawake?
Joel: Ninatongozwa kila siku, siwezi kusema ni idadi gani ya wanawake lakini ni wengi lakini si jambo ambalo ninaliweka maanani.
DIMBA:Kuna tetesi zilisambaa kuwa ulikuwa unatoka kimapenzi na Muna Love kwako lipoje?
Joel: Hapa sijawahi kuwa naye kimapenzi, Muna ni mtu ambaye tunafahamiana tu lakini kusambaa kwa picha zangu na ye ye kwenye mitandao ya kijamii haimaanishi tuoo kwenye mahusiano.
DIMBA: Je yule mtoto wake alikuwa wako?
Joel:Hapana, sijawahi kuwa na mtoto katika maisha yangu, yule alikuwa mtoto wake ana alikuwa na baba yake.
DIMBA: Je unapenda kunyoa mitindo gani?
Joel: Mitindo yoyote kwa sababu hakuna kinachonizuia mimi kunyoa ninavyotaka ,kwa sababu simkwazi mtu.
Ninapenda kuonekana mtanashati kwasababu haitaondoa maana ya kila ninachokifanya.
DIMBA:Nywele zako unatumia mafuta yaa bei gani kuziremba?
Joel: Ni 8000 tu,sikumbuki yanaitwaje lakini hayazidi kiasi hicho cha fedha.
DIMBA:Unavaa saa ya bei gani?
Joel: Saa zangu zinaanzia shilingi 45,000 hadi laki 2.
DIMBA: Suti zako unazovaa unashona kwa bei gani?
Joel: Haipungui chini ya laki 8, kwasababu inategemea na ubora wa vitambaa na fundi ambaye atashona hiyo suti.
DIMBA:Ni shoo gani ambayo umewahi kufanya ukalipwa fedha kidogo sana?
Joel: Mara nyingi nafanya bure, unanikuta kuna watu wengine wanakuhitaji lakini hakuna fedha inabidi niendele ni fanye tu.
DIMBA: Je ulishawahi kutamani kuwa mwanasiasa?
Joel: Wakati nilipokuwa shule ya Msingi nilitamani kuwa mwanasiasa kutokana na nafasi za uongozi ambazo nilikuwa napewa.
Wanafunzi walikuwa wananishikiniza nikiwa mkubwa niwe mwanasiasa lakini baadae nilibadili mawazo na kuingia kwenye uimbaji.
DIMBA:Ni msanii gani wa bongo fleva ambaye unamkubali?
Joel: Wapo wengi lakini ni Ali Kiba na Ben Pol, ni wasanii ambao muda mwingine wanaomba nyimbo ambazo zinagusa maisha ya watu na pia zinawatia moyo kwa kile wanachokifanya.
DIMBA: Ni nyimbo gani ya Ben Pol unayoikubali?
Joel: Ni wimbo wake wa Bado kigodo, ni nyimbo ambayo ukiisikiliza inakupa hamu ya kupambana kwa ajili ya kutafuta fedha za kutunza familia.
DIMBA: Ni msanii gani wa bongo fleva ambaye anakukubali?
Joel: Kuna kipindi nilikuwa nasafiri lakini nilivyofika Airpot nikakutana na Diamond Platnumz, alinisimamisha na kuniambia kuwa ananikubali kutokana na kazi zangu ninazofanya.
Aliniambia kuwa yeye ni shabiki yangu mkubwa katika nyimbo zangu, na pia huwa akienda kwenye vyombo vya habari huwa anaomba nyimbo zangu zipigwe.
DIMBA:Je ungependa kuwa na watoto wangapi katika maisha yako?
Joel: Kwetu tumezaliwa wanne kwahiyo na mimi ningependa kuwa na watoto wanne.
DIMBA:Ahsante kwa ushirikiano wako
Joel:Shukrani sana.

The post JOEL LWAGA Mkali wa Injili anayemzimia Diamond Platinum appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *