Posted By Posted On

KAZE ATUMIWA FAILI LA WACHEZAJI YANGA

NA WINFRIDA MTOI ZIKIWA zimebaki siku chake kabla ya pambano la watani wa jadi, kocha mpya wa Yanga, Cedric C, ametumiwa faili la wachezaji wa timu hiyo na mwenendo wa programu za kocha mtangulizi wake, Zlatko Krmpotic, aliyetimuliwa. Kocha huyo raia wa Burundi anakuja kuchukua nafasi ya Zlatko aliyesitishiwa mkataba baada ya kuiongoza Yanga katika
The post KAZE ATUMIWA FAILI LA WACHEZAJI YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA WINFRIDA MTOI

ZIKIWA zimebaki siku chake kabla ya pambano la watani wa jadi, kocha mpya wa Yanga, Cedric C, ametumiwa faili la wachezaji wa timu hiyo na mwenendo wa programu za kocha mtangulizi wake, Zlatko Krmpotic, aliyetimuliwa.

Kocha huyo raia wa Burundi anakuja kuchukua nafasi ya Zlatko aliyesitishiwa mkataba baada ya kuiongoza Yanga katika mechi tano ndani ya siku 37.

Sababu kubwa iliyomuondoa kocha huyo inaelezwa ni uongozi kutoridhishwa na mwenendo wa mbinu zake na tayari Kaze ametumiwa faili lenye mahitaji yote Yanga inayohitaji ndani ya uwanja.

Ukiachana na mbinu, inadaiwa sababu nyingine iliyomuondoa Zlatko mapema ni program zake za mazoezi zinazowafanya wachezaji wasiwe fiti licha ya kuwa na viwango bora.

Kwa kawaida, utaratibu wa timu nyingi huwa zinafanya mazoezi saa mbili, lakini inadaiwa kuwa Zlatko alikuwa akifanya programu ya dakika 60, wakati uwanjani wanacheza 90.

Inadaiwa kuwa ubishi wa kocha huyo, ulimfanya kuingia katika mvutano wa mara kwa mara kuanzia viongozi wenzake wa benchi la ufundi hadi wachezaji.

Kutokana na hamu ya Wanajangwani hao kutaka kuona kikosi chao kinaimarika mapema, ukizingatia imefanya usajili wa gharama, wameamua kumpa baadhi ya vitu muhimu Kaze ili kabla ya kutua nchini aanze navyo fasta.

Kocha huyo anayetarajiwa kuwasili siku yoyote kuanzia leo, atakuja kuanza na pambano la watani wa jadi linalotarajia kupigwa Jumapili ya wiki ijayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Habari ambazo DIMBA Jumatano imezipata kutoka ndani ya Yanga, zinasema kocha huyo, ametumiwa dondoo muhimu za kikosi hicho na viwango vya wachezaji walivyoonesha tangu ligi imeanza.

Mtoa habari huyo, alisema ilikuwa kocha huyo atume programu ianze kufanyika kazi na makocha waliopo, lakini wanasubiri asaini mkataba kabisa.

“Siku yoyote Kaze anaweza kuwasili, kila kitu anakijua kwa sababu amepewa mkanda mzima wa kile uongozi unahitaji na vikao vilivyofanyika amekuwa akishiriki kwa njia ya mtandao.

“Ujue huyu kocha ndiye tuliyekuwa tunamtaka tangu mwanzo, hivyo imekuwa rahisi kamati kumpitisha, kuna vitu ameviomba, vyote ametumiwa,” kilisema chanzo hicho.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya usajili, Hersi Said, moja ya kigezo kilichowafanya kumchukua kocha huyo ni kutokana na taaluma yake na kuzungumza lugha nyingi.

Hersi alisema, kumekuwa na changamoto iliyokuwa inawakabili wachezaji wengi wanaotoka nchi mbalimbali kupata shida katika eneo la lugha lakini Kaze atakuja kumaliza tatizo hilo.

“Kaze anatoka kituo chenye taaluma ya soka, anazungumza lugha tofauti kwa ufasaha kama vile Kiswahili, Kifaransa, Kihispania, hii itatutasaidia kwa sababu tuna wachezaji kutoka nchi mbalimbali,” alisema.

Alieleza kuwa wanahitaji kocha ambaye atawafanya wachezaji wafurahie na kujengwa kisoka na kisaikolojia kuanzia ngazi ya chini.

The post KAZE ATUMIWA FAILI LA WACHEZAJI YANGA appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *