Posted By Posted On

Mjue Kobe Bryant (11):Aliitwa NBA All-Rookie akiwa na umri mdogo

Na Badi Mchomolo HUU ni mwendelezo wa simulizi ya nyota wa zamani wa mchezo wa kikapu nchini Marekani, Kobe Bryant, aliyefariki dunia Januari 26, mwaka huu Calabasas, California, akiwa na umri wa miaka 41. Hii ni safu ambayo inaweza kukufanya ukayajua vizuri maisha ya staa wako, kama ndio kwanza unaungana nami basi hii ni sehemu
The post Mjue Kobe Bryant (11):Aliitwa NBA All-Rookie akiwa na umri mdogo appeared first on Gazeti la Dimba.,

Na Badi Mchomolo

HUU ni mwendelezo wa simulizi ya nyota wa zamani wa mchezo wa kikapu nchini Marekani, Kobe Bryant, aliyefariki dunia Januari 26, mwaka huu Calabasas, California, akiwa na umri wa miaka 41.

Hii ni safu ambayo inaweza kukufanya ukayajua vizuri maisha ya staa wako, kama ndio kwanza unaungana nami basi hii ni sehemu ya 11 ya simulizi ya nguli huyo wa kikapu.

Wiki iliopita sehemu ya 10, tuliona jinsi mchezaji huyo alivyopata taabu kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya Los Angeles Lakers huku akiwa na umri wa miaka 18.

Kwa kukukumbusha kidogo ni kwamba, mchezaji huyo alipata ugumu wa kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza kutokana na namba yake aliyokuwa anacheza ilikuwa inatumiwa na mastaa wawili ambao walikuwa kwenye uwezo mkubwa kwa wakati huo Eddie Jones pamoja na Nick Van Exel.

Hao walikuwa wachezaji wakongwe kwenye kikosi hicho Jones alijiunga na matajiri hao tangu mwaka 1994 kabla ya kuondoka mwaka 1999, wakati huo Van Exel alikuwa hapo tangu mwaka 1993 hadi 1998.

Wote hao walikuwa wanacheza nafasi ya Shooting Guard, lakini Jones alikuwa na uwezo pia wa kucheza Small Forward, hivyo Bryant muda mwingi alikuwa benchi kwa ajili ya kujifunza na kutoka kwao.

…Tuachane na habari hiyo, leo tunaangalia jinsi alivyoingia kwenye kikosi cha NBA All-Rookie Second Team, huku akiwa na umri wa miaka 18.

Mbali na kutopata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza ndani ya Los Angeles Lakers, alifanya mazoezi ya nguvu na kushiriki michuano mingine ambayo sio ya Ligi Kuu, kama vile Rookie Challenge na All-Star weekend.

Huku nako kulimsaidia sana, aliweza kuonesha kile anachojifunza kutoka kwa Eddie Jones pamoja na Nick Van Exel ambao wamekuwa wakimuweka benchi.

Baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya Rookie Challenge, alifanikiwa kutwaa tuzo ya Slam Dunk Contest.

Slam Dunk ni shindano la kila mwaka la Chama cha Mpira wa Kikapu la kitaifa linalofanyika wakati wa Wiki ya mashindano ya Nyota wa NBA.

Hapo nyota wa kikapu wanashindani jinsi ya kupachika kikapu kwa aina tofauti za kuruka juu, hivyo Bryant alishinda na kutwaa tuzo hiyo.

Mbali na tuzo hiyo, aliandika historia ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kushinda tuzo hiyo huku akiwa na umri wa miaka 18.

NBA All-Rookie Second Team ni timu ambayo inakuwa na wachezaji bora watano na wachezaji hao uchaguliwa na makocha wa timu tofauti na anakotoka mchezaji husika.

Hivyo katika majina matano lilikuwepo la Bryant pamoja na rafiki yake kutoka Los Angeles Lakers, Travis Knight ambaye pia alikuwa anasugua naye benchi Lakers. Hapo nyota ya Bryant ilianza kung’ara mara baada ya kuitwa kwenye kikosi hicho.

Uongozi wa timu ya Lakers ulimpongeza na kumuhakikisha namba kwenye kikosi cha kwanza bila ya kujali uwepo wa wapinzani wake wawili. Tukutane wiki ijayo kuona jinsi gani alipata namba Los Angeles Lakers.

The post Mjue Kobe Bryant (11):Aliitwa NBA All-Rookie akiwa na umri mdogo appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *