Posted By Posted On

MTIHANI HUU Cavani kuirudisha namba 7 kwenye ramani Old Trafford?

MANCHESTER, England EDINSON Cavani amejiunga na Manchester United siku ya m wisho ya usajili akiwa huru. Straika huyo raia wa Uruguay ameingia Old Trafford baada ya kuitumikia PSG kwa miaka saba ambako alifunga mabao zaidi ya 200. Baada ya kumkosa Jadon Sancho wa Borussia Dortmund, mabingwa wa zamani wa England walimnasa Cavani mwenye umri wa
The post MTIHANI HUU Cavani kuirudisha namba 7 kwenye ramani Old Trafford? appeared first on Gazeti la Dimba.,

MANCHESTER, England

EDINSON Cavani amejiunga na Manchester United siku ya m

wisho ya usajili akiwa huru. Straika huyo raia wa Uruguay ameingia Old Trafford baada ya kuitumikia PSG kwa miaka saba ambako alifunga mabao zaidi ya 200.

Baada ya kumkosa Jadon Sancho wa Borussia Dortmund, mabingwa wa zamani wa England walimnasa Cavani mwenye umri wa miaka 33 na kumkabidhi jezi namba 7 ambayo ina historia kubwa ndani ya klabu hiyo.

Je, atafanikiwa kufuata nyayo za magwiji kama George Best, Eric Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo ambao waliweka alama nzuri wakiwa na jezi namba 7 ndani ya Old Trafford?

Lakini, wapo walioshindwa kuitendea haki jezi hiyo kama ilivyokuwa kwa Angel Di Maria, Memphis Depay, Michael Owen na Alexis Sanchez.

Kwa zaidi ya miaka 50, jezi namba 7 ni alama ya Manchester United. Lakini, tangu Ronaldo aondoke miaka 11 iliyopita, hakuna aliyeweza kufanya makubwa akiwa na jezi hiyo.

Cavani ataweza kuvunja mwiko walioushindwa akina Sanchez na kurudisha heshima ya namba 7 kama alivyokuwa Ronaldo ndani ya Old Trafford?

ALEXIS SANCHEZ (2018-2020)

Baada ya kufanya vizuri kwa misimu minne akiwa na Arsenal, Sanchez aliondoka Emirates na kwenda Old Trafford ambako alitabiriwa kufanya makubwa kama ilivyokuwa kwa Washika Bunduki.

Straika Robin van Persie alifanikiwa kuwa staa mkubwa wa Manchester United kutoka Arsenal.

Hata hivyo, winga huyo raia wa Chile alishindwa kufanya vizuri, aliishi kwenye kivuli chake, hakuweza kufika malengo ya Manchester United.

Alifunga mabao matano katika michezo 45 aliyocheza, sasa amejiunga jumla na Inter Milan baada ya kutolewa kwa mkopo msimu uliopita.

MEMPHIS DEPAY (2015-2016)

Haraka Memphis Depay alipewa jezi namba 7 na kocha Louis van Gaal baada ya kusajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 25 kutoka PSV.

Lakini, hakuweza kufanya chochote bora na jezi hiyo tangu alipowasili kutoka Uholanzi. Baada ya miezi 12 winga huyo wa Kidachi kutolewa kwa mkopo na kuuzwa jumla kwenda Lyon ambako alianza kufanya vizuri na kurejea kwenye makali yake.

MICHAEL OWEN (2009-2012)

Michael hakuwa mchezaji mbaya, lakini, jezi namba 7 ilimzidi uwezo.

Katika dunia ya mpira, Lionel Messi pekee ndiye alikuwa na uwezo wa kuziba pengo la Ronaldo lililoachwa mwaka 2009 baada ya kuondoka Old Trafford.

Owen aliyekuwa akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara aliachwa huru na Newcastle United ambao walishuka daraja, ghafla straika huyo aliyekuwa na miaka 30 alisajili na Manchester United baada ya kumkosa Karim Benzema.

Alijitahidi kiasi, anakumbukwa kwa kufunga bao la ushindi dhidi ya Manchester City, kufunga bao la ushindi katika fainali ya Kombe la Ligi na kufunga mabao matatu ‘hat trick’ katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini hakukaribia kiwango cha kuvaa jezi namba ya Manchester United.

ANGEL DI MARIA (2014-2015)

Licha ya kusajiliwa kwa dau kubwa la pauni milioni 59.1 na kuweka rekodi nchini England, Di Maria alishindwa kufanya vizuri Manchester United.

Di Maria aliwasili Old Trafford kutoka Real Madrid ambako alitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, tena akiwa nyota wa mchezo katika mechi ya fainali.

Mwanzo ulionekana kuwa usajili mzuri. Ghafla, kiwango chake kilishuka na baada ya msimu kumalizika aliuzwa PSG kwa dau la pauni milioni 44.

The post MTIHANI HUU Cavani kuirudisha namba 7 kwenye ramani Old Trafford? appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *