Posted By Posted On

Mugalu anacheza na goli la Yanga

NA JESSCA NANGAWE STRAIKA wa Simba, Chris Mugalu, ameanza moto wake baada ya kuongeza kasi ya mazoezi ya ziada ili kujiwinda na michezo ya Ligi Kuu Bara ikiwemo dhidi ya wapinzani wao Yanga. Simba ambayo inakamata nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia alama 13 itakua mgeni katika pambano lao dhidi ya watani zao Yanga Oktoba 18.
The post Mugalu anacheza na goli la Yanga appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA JESSCA NANGAWE

STRAIKA wa Simba, Chris Mugalu, ameanza moto wake baada ya kuongeza kasi ya mazoezi ya ziada ili kujiwinda na michezo ya Ligi Kuu Bara ikiwemo dhidi ya wapinzani wao Yanga.

Simba ambayo inakamata nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia alama 13 itakua mgeni katika pambano lao dhidi ya watani zao Yanga Oktoba 18.

Miongoni mwa nyota wanaozungumzwa sana ndani ya kikosi cha Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, ni pamoja na straika huyo ambaye ameonyesha uwezo mkubwa ikiwa ni msimu wake wa kwanza tangu aliposajiliwa akitokea ligi ya Zambia.

Mugalu ameendelea kuwa tishio ndani ya kikosi cha Simba baada ya kuendelea kuipatia timu hiyo mafanikio akiwa ni miongoni mwa wachezaji tegemeo kikosini hapo.

Wakati kikosi cha Simba kikitarajiwa kuingia kambini Jumatatu ijayo kujiwinda na mchezo wao dhidi ya Yanga, straika huyo yeye ameendelea kujifua kivyake ili kujiweka fiti zaidi.

Hata hivyo nyota ya straika huyo imeendeela kung’a ambapo mpaka sasa tayari ameshaifungia timu yake mabao matatu akiongozwa na mwenzake Meddie Kagere mwenye mabao manne hadi sasa.

Uwezo wake umeendeela kumfanya kupewa nafasi kubwa ndani ya kikosi cha kwanza na hivyo kutegemewa kwa kiasi kikubwa kuleta mafanikio kikosi hapo.

Kocha mkuu wa timu hiyo alisisitiza kuwa kila mchezaji ndani ya timu hiyo anapaswa kufanya majukumu yake na kila mchezaji anatakiwa kufunga kwa kuwa ni jukumu la wote.

The post Mugalu anacheza na goli la Yanga appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *