Posted By Posted On

SIMBA NA YANGA HATARINI KUAHIRISHWA TENA KWA SABABU YA MECHI YA TAIFA STARS NA TUNISIA KUFUZU AFCON

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

KUNA uwezekano mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga uliosogezwa Novemba 7 kutoka Oktoba 18 ukasogezwa tena mbele.

Hiyo ni baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutoa ratiba ya mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika leo (AFCON), ikionyesha Tanzania itamenyana na Tunisia Novemba 13 Jijini Tunis katika mchezo wa Kundi J.

Na kwa sababu timu hizo zitarudiana Novemba 13 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, basi mchezo huo unaweza kufanyika kuanzia mwishoni mwa mwezi Novemba.


Mapema leo Bodi ya Ligi ilitoa taarifa ya kuusogeza mbele mchezo huo hadi Novemba 7 kwa hofu ya wachezaji waliokwenda kuchezea timu zao za taifa kuchelewa kurudi kwa sababu mbalimbali, ikiwemlo vikwazo vya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.   

Lakini kwa kuwa Novemba 13 Taifa Stars itacheza na Tunisia Jijini Tunis, itahitaji angalau wiki moja ya maandalizi, hivyo ni vigumu mechi ya Simba na Yanga kuchezwa Novemba 7.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *