Posted By Posted On

SVEN AFUATA SUMU YA YANGA ZANZIBAR

NA JESSCA NANGAWE WAKATI homa ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga likianza kupamba moto kila kona, kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, yupo zake Zanzibar akipanga hesabu zake za ushindi. Simba na Yanga zinatarajia kukutana Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mchezo wao wa mzunguko wa
The post SVEN AFUATA SUMU YA YANGA ZANZIBAR appeared first on Gazeti la Dimba.,

NA JESSCA NANGAWE

WAKATI homa ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga likianza kupamba moto kila kona, kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, yupo zake Zanzibar akipanga hesabu zake za ushindi.

Simba na Yanga zinatarajia kukutana Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam ikiwa ni mchezo wao wa mzunguko wa kwanza Ligi Kuu Bara na pia itakua ni mchezo wao wa kwanza kufuatia ligi kusimama kwa muda kupisha mechi za timu ya taifa ambapo Taifa Stars inacheza na Burundi.

Tambo mbalimbali zimeanza kumiminika kwa mashabiki wa timu hizo huku kila moja ikijinasibu kuibuka na alama tatu muhimu.

Wakati tambo hizo zikiendelea kocha wa Simba ameamua kwenda kujipumzisha visiwani humo huku akitarajia kuanza programu ya mazoezi Jumatatu ijayo ili kujiweka fiti na michezo inayoendelea ya ligi hiyo.

Sven sambamba na kocha wa viungo, Adel Zrane, walionekana visiwani humo huku sababu kubwa ikitajwa kwenda kupumzika pamoja na kuweka mipango sawa tayari kwa pambano hilo muhimu kwao.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Sven alisema, licha ya ukubwa wa mchezo huo hana anachokihofia kwani wachezaji wake ni watu wenye kujitambua na ana uhakika wa kuichapa Yanga.

“Tunajiandaa na michezo yote iliyo mbele yetu, kila mchezo ni muhimu, tunataka kushinda michezo yote kwenye ligi kwa lengo la kuulinda ubingwa wetu kwa mara nyingine tena,” alisema Sven.

The post SVEN AFUATA SUMU YA YANGA ZANZIBAR appeared first on Gazeti la Dimba.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *