Posted By Posted On

Grammy wampa heshima hii Diamond Platnumz

NA CHRISTOPHER MSEKENA

NYOTA wa muziki nchini, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameendelea kuandika historia baada ya kuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kufanyiwa mahojiano maalum na waandaaji wa tuzo kubwa za muziki duniani, Grammy.

Kupitia tovuti na kurasa zao za mitandao ya kijamii, Grammy wamemtaja Diamond kama mwanamuziki aliyeweza kubadilisha taswira ya muziki wa Afrika Mashariki na kufika viwango ambavyo ni ndoto ya kila msanii barani humu.

Katika mahojiano hayo ambayo yanahusu mambo kadha wa kadha kuhusu muziki wake hasa kufanya kolabo kubwa na mastaa orodha A ulimwenguni kama vile Rick Ross, Omario, Ne-Yo na kushiriki katika albamu, ALICIA ya Alicia Keys.

Akizungumzia ukubwa wake na jinsi anavyoweza kulinda heshima yake, Diamond alisema: “Ni baraka ila ni vigumu kwa sababu inatakiwa nihakikishe nakilinda kila nilicho nacho, sihitaji kuwaangusha mashabiki zangu, nahakikisha nafanya kazi zaidi na kutengeneza nyimbo za ladha tofauti, nikiwa jukwaani nahikikisha nafanya kwa uwezo wangu, ni mambo ambayo yananifanya siwezi kupumzika kabisa.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *