Posted By Posted On

Joh Makini amsaini Otuck William

NA JEREMIA ERNEST

MKALI wa Hip hop nchini, Joh Makini, ametambulisha lebo yake mpya Makini Record pamoja na msanii wa kwanza, Otuck William.

Akizungumza na waandishi jana jijini Dar es Salaam, Joh alisema Makini Record wana mpango wa kusaidia vipaji vingi ila kwa kuanza wamemtambulisha Otuck William ambaye si jina geni kwa mashabiki wa muziki mzuri.

“Namtambulisha lebo yangu ya Makini Record na msanii wangu mpya Otuck William ambaye ni mwimbaji wa Bongo Fleva na leo (jana) tunaachia ngoma mpya ambayo tumefanya pamoja inaitwa Mbele kwa Mbele,” alisema Joh Makini.

Otuck ni miongoni mwa wasanii wakali wa RnB hapa nchini ambapo nje ya muziki amekuwa akifanya kazi na taasisi na mashirika ya ndani na nje nchi.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *