Posted By Posted On

MSOLLA AWATAKA WACHEZAJI KUENDLEZA MAPAMBANO

Msomaji wa Yanganews Blog:Mwenyekiti Dkt. Mshindo Msolla amezungumza na viongozi wa benchi la ufundi na wachezaji katika kikao maalumu cha mabadiliko katika timu ya Wananchi baada ya kuondolewa kwa kocha mkuu Zlatko Krmpotic.

Dkt. Msolla amesema mabadiliko ya makocha ni jambo la kawaida kwa timu inayohitaji mafanikio hivyo wachezaji na makocha wengine wasiingiwe na unyonge.

“Kuondoka kwa kocha isiwe sababu ya kuwatia unyonge, muhimu ni kwamba mliopo tunaamini katika uwezo wenu hivyo muendeleze kazi nzuri wakati huu ambao anatafutwa kocha mkuu mwingine”.

” Kwa wachezaji hili lisiwatie wasiwasi mnafahamu kuwa timu inayohitaji mafanikio na inayojijenga kuna wakati inapitia katika hatua ngumu kama hizi , ” amesema .

Aidha Dkt . Msolla amewataka Wanachama , Wapenzi na Mashabiki wa Yanga , kuendelea kuwaunga mkono viongozi na kuisapoti timu yao kwa hali na mali katika kipindi hiki ambacho wanapambania kurejesha heshima Jangwani .

,,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *