Posted By Posted On

Mwadui wapanga kuitibulia Azam

NA VICTORIA GODFREY

BAADA ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo  uliochezwa  wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi, Kocha wa Mwadui, Khalid Adam amesema wanajipanga kutibua rekodi ya Azam.

Azam kwa sasa wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 15, wakiwa hajapoteza ambao wanataraja kucheza na Mwadui Oktoba 15, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Adam alisema wanaendelea kujipanga  ili kuhakikisha wanaifunga Azam katika uwanja wao wa nyumbani na kutibua rekodi yao.

“Ratiba zote za maandalizi yetu itajulikana  kesho (leo), tumewasili Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wetu dhidi na Azam,” alisema Adam.

Adam alisema mipango  yao mingine ya kuhakikisha wanafanya vyema mchezo huo  itafanyika leo baada ya kutua  Dar es Salaam. Mwadui wanashika nafasi ya nane katika mchezo wa ligi hiyo inayoshirikisha timu 18 kutokana na sita baada ya kushinda mara mbili na  kupoteza mitatu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *