Posted By Posted On

Ndayiragije akili zake zote kwa Tunisia

NA ZAINAB IDDY

LICHA ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kukabiliwa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam, Kocha wa kikosi hicho, Ettiene Ndayiragije, amesema akili yake ipo Tunisia.

Taifa Stars wanatarajia kucheza na Tunisia ugenini Novemba 13, mwaka huu na baadaye kurudiana Novemba 17, kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dares Salaam, ukiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) itakazofanyika mwakani Cameroon.

Katika michuano hiyo, Tanzania imepangwa Kundi J, pamoja na Tunisia, Equatorial Guinea na Libya, ambapo mchezo wa kwanza uliochezwa mwaka jana, kwenye Uwanja wa Mkapa, Taifa Stars iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Equatorial Guinea, kabla ya kufungwa mabao 2-1 na Libya  mtanange uliochezwa nchini Morocco.

Akizungumza na BINGWA, jijini Dar es Salaam jana, Ndayiragije ambaye ni raia wa Burundi  alisema mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi hauna umuhimu mkubwa wa kupata matokeo bora kama ile dhidi ya Tunisia.

“Mechi na Burundi kwangu ni kipimo cha kuangalia nina wachezaji wa aina gani wa kwenda nao nchini Tunisia ambako ndiko kuna menchi ngumu na muhimu kwa nchi.

“Hata nilipowaomba TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) wanitafutie mchezo mmoja wa kirafiki kulingana na kalenda ya shirikisho la Soka Kimataifa (FIFA) sikutaka watumie nguvu kubwa kuzishawishi timu bali niliwaambia nchi yoyote itakayokuwa tayari kucheza nasi  tutacheza nayo,” alisema Ndayiragije

Ndayiragije alisema mchezo na Burundi utampa mwanga na nini atatakiwa kufanya ili kuwa na timu itakayotoa changamoto mbele ya Tunisia.

“Baada ya mechi yetu na Burundi nao Tunisia watakuwa na mchezo wa kirafiki na itakuwa nafasi yangu ya kuangalia nini wanafanya, kisha kulinganisha na kile kitakachojitokeza Stars dhidi ya Burundi na kuanza mpango wa kujenga timu ya ushindani,” alisema.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *