Posted By Posted On

NIKABIDHINI :Cavani atajivunia kuvaa jezi namba 7

MANCHESTER, England

EDINSON Cavani amesema yuko tayari kwa majukumu yanayotokana na kuvaa jezi namba saba ya Manchester United.

Straika huyo aliyesaini mkataba wa miaka miwili Old Trafford Jumatatu, atafuata nyayo za Eric Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo kwa kurithi jezi namba 7 ya Man United na licha ya kuwa na umri wa miaka 33, amedhamiria kutimiza matarajio yatokanayo na ukubwa wa namba ya jezi hiyo.

“Itanipa fahari kuvaa jezi namba 7 ya Manchester United,” alisema Cavani raia wa Uruguay aliyejiunga na Mashetani Wekundu siku ya mwisho ya dirisha la usajili.

“Sasa naenda kujiandaa na majukumu haya, nifanye kila niwezalo niwe tayari na kufurahia na ninaimani ya kuwacha alama Manchester United.

“Nina miaka miwili ya mkataba na Manchester United. Nataka nijitoe kamili nikiwa hapa. Najihisi furaha.”

Cavani amekuwa mchezaji huru tangu kuondoka Paris Saint-Germain na hajacheza soka la ushindani tangu Machi.

Hakuichezea PSG wakati wa michuano mifupi ya Klabu Bingwa Ulaya iliyofanyika Ureno na alidhibitisha kuambukizwa Covid-19 akiwa mapumzikoni na mchumba wake.

“Hakukua na haja ya kumwambia mtu yeyote au kusema chochote,” alisema Cavani.

“Ingekua tofauti kama ningekuwa ninacheza, lakini imetokea baadaya kuchukua mapumziko Hispania. Baada ya kuwasili Paris, tulipimwa na kugudulika hatuna maamubuzi.

“Lakini baadaye, mchumba wangu alionyesha dalili na tukarudia vipimo na akagundulika ameambukizwa, na kwa sababu alikua nayo, pia mimi nikawa nayo. Naongea kuhusu hiyo kwa sababu tayari imeshafanyika.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *