RASMI, LAMINE MORO APEWA UNAHODHA YANGA
Msomaji wa Yanganews Blog: Beki wa mabingwa wa kihistoria Yanga, Lamine Moro rasmi ameteuliwa kuwa nahodha wa Yanga.
Pia katika uteuzi huo, naye beki Bakar Nondo Mwamnyeto ameteuliwa kuwa nahodha msaidizi.
Afisa habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema Lamine ndio anakuwa nahodha mkuu na msaidizi wake ni Mwamnyeto wakati nahodha namba tatu atakuwa Mukoko Tonombe.
“Ni uamuzi wa benchi la ufundi na umezingatia mambo mengi, ikiwemo nidhamu ya wachezaji kwenye kikosi” amesema Bumbuli
Amesema benchi la ufundi limependekeza majina hayo kwa uongozi na baada ya kikao kati ya benchi la ufundi na viongozi, uongozi haukuwa na pingamizi ya mapendekezo hayo.
,,
Comments (0)