Posted By Posted On

AZAM: TUPO TAYARI KUENDELEA NA LIGI

NA VICTORIA GODFREY

KLABU ya Azam ipo tayari kuendelea na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui utakaochezwa Oktoba 15, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Kauli hiyo imekuja baada ya Bodi ya Ligi Tanzania kusogeza mbele mchezo wa Simba na Yanga uliopangwa kucheza Oktoba 18, mwaka huu na sasa utapigwa Novemba 7, kwenye Uwanja wa Mkapa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na bodi hiyo, uamuzi huo ulitokana na wachezaji wa kigeni wa Simba na Yanga ambao wamekwenda kuzitumikia timu zao za taifa kuweza kuathiri klabu hizo, kwani kikwazo cha usafri bado kwa baadhi ya nchi ambazo hazijafungua mipaka kwa hofu ya corona. Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Klabu ya Azam, Thabit Zakaria, alisema hawahitaji mchezo huo kusogezwa mbele kama ilivyo wa Simba na Yanga. Zakaria alisema pamoja na wachezaji kuondoka na kwenda katika vikosi cha taifa ya nchi zao, akiwamo Mganda Nicolus Wadada na Mghana Yakubu Mohamed, hawana tatizo na ratiba ya ligi hiyo. Alisema wanaweza kuendelea kucheza michezo yao ya Ligi Kuu Bara bila wachezaji hao wawili wa kigeni na kupata matokeo mazuri. Zakaria alisema wanaendelea kujipanga kuhakikisha wanafanya vyema na kupata matokeo mazuri katika michezo yao ya ligi kwani malengo yao ni kutwaa ubingwa msimu huu. “Sisi kwa upande wetu hatuna shida na tuko tayari kwa michezo yetu, tukianzia huu wa Oktoba 15 , ingawa tuliahidiwa hadi kufika Oktoba 13, wachezaji wetu wamekuwa wamerejea kutikana na ratiba ya usafiri wa ndege,” alisema Zakari.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *