Posted By Posted On

Djokovic huyoo nusu fainali French Open

PARIS, Ufaransa

MCHEZA tenisi Novak Djokovic, amefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Wazi ya Ufaransa (French Open) baada ya kumshinda Pablo Carreno-Busta katika mchezo wa robo fainali jana.

Mchezaji huyo namba moja wa tenisi duniani,  alianza kwa kuteswa na Pablo

Carreno-Busta, kabla ya kuzinduka na kushinda 4-6, 6-2, 6-3, 6-4.

Baada ya kufungwa, Muhispania huyo ambaye alikuwa ni mpinzani wa Djokovic katika michuano ya US Open, alisema presha ya mchezo huo ndiyo iliyomgharimu. 

“Sifahamu, labda ni presha au kitu kingine. Lakini, ninamaanisha, anacheza kawaida tu,” alisema.

Kwa upande wake, Djokovic aliviambia vyombo vya habari vya Serbia kwamba shingo yake ilitakiwa kutibiwa kabla ya mchezo huo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *