Posted By Posted On

KMC yaipeleka Yanga CCM Kirumba

NA ZAINAB IDDY KLABU ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imepanga kucheza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga  kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza badala ya ule wa Uhuru,jijini, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa ratiba ya mabadiliko ya ligi hiyo iliyotolewa juzi,  raundi ya sita, saba na nane  inaonesha KMC watakuwa wenyeji wa  Yanga Oktoba 25, mwaka huu. Tangu kuanza kwa msimu huo,  KMC  wamecheza michezo  tano  na mitatu walikuwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam. Katika mchezo wa kwanza, KMC iliibuka na ushindi wa mabao  4-0 dhidi ya Mbeya City na baadaye  2-1 dhidi Tanzania Prisons  kabla ya kufungwa bao 1-0 na Polisi Tanzania. Akizungumzia mabadiliko hayo ya uwanja ya KMC, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo alisema moja ya kanuni zilizopo katika ligi kuu msimu huu ni timu shiriki kupewa nafasi ya kuchagua michezo miwili ambayo itacheza kwenye uwanja ambao ni chaguo lao tofauti na uwanja wa nyumbani waliochagua awali. “Kutokana na kanuni hiyo,  KMC wameomba kwenda kucheza mechi yao na Yanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kutokana na kuwa mchezo huo unaingiza idadi kubwa ya mashabiki. “Kutokana na chaguo hilo, Bodi tumeridhia mapendekezo yao na kuwapa taarifa Yanga juu ya kutakiwa kwenda Mwanza  pale muda utakapofika wa kwenda kucheza dhidi ya KMC,” Kasongo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *