Posted By Posted On

UCHOKOZI: Liverpool, Bayern Munich zajitosa kuitibulia Man United kwa Sancho

DORTMUND, Ujerumani

MSHAMBULIAJI wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho, kwa sasa anaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kujiunga na Liverpool au Bayern Munich badala ya Manchester United, imeripotiwa.

United ilimfanya Sancho kama chaguo lao namba moja katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wa kiangazi, lakini pamoja na miezi kadhaa kupita, wameshindwa kukubaliana na matakwa ya BVB.

Japo Mashetani Wekundu hao walipuuzia tarehe ya mwisho iliyowekwa na Dortmund ambayo ni Agosti 10 kukamilisha uhamisho huo, klabu hiyo inaamini dili hilo litafanikiwa.

Inafahamika, Sancho alikuwa tayari kutua Old Trafford na tayari alishakubaliana na maslahi binafsi na klabu hiyo.

Kipindi hiki cha usajili wa kiangazi kilionekana ni sahihi kwa United kumsajili Sancho. Si tu alionekana ni mchezaji muhimu wa kuisaidia United na kuifikisha katika kiwango cha juu, pia klabu hiyo ni miongoni mwa chache zilizokuwa na uwezo wa kulipa fedha iliyotakiwa kumtwaa mkali huyo.

Mwisho wa siku, wameamua kutokutana na Dortmund na badala yake, kuangalia kwingineko.

Habari zilizopatikana juzi na jana, zinadai kuwa ikiwa ni siku chache kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, Liverpool na Bayern zimejitosa kuipiku United katika mbio za kuinasa saini ya nyota huyo.

Ripoti zinasema kuwa Sancho alikuwa tayari kujiunga na Manchester, lakini fedha iliyotakiwa na klabu yake ndiyo iliyokwamisha dili hilo.

Mchezaji huyo na wakala wake wote wamekuwa kimya juu ya majaliwa ya Sancho, lakini United walishindwa kufanya kile walichotakiwa ili kupata huduma yake.

Matokeo yake, Bayern au Liverpool kwa sasa inaonekana huenda yakawa makazi ya mchezaji huyo msimu ujao.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, aliwahi kuzungumza na Sancho na wakati Mashetani Wekundu wakihusishwa naye, klabu hiyo isingekuwa tayari kutoa pauni milioni 108 kwa ajili ya nyota huyo.

Na sasa kilichobaki ni kuona mchezaji huyo akitua Bayern au Liverpool, lakini kilichopo wazi ni kwamba United wamepoteza nafasi adimu ya kumtwaa Sancho kutokana na kupuuza mahitaji ya Dortmund.

Akiwa na umri wa miaka 20 tu, Sancho si tu mmoja wa wachezaji chipukizi wenye vipaji wanaovutia, lakini amejitambulisha kama mmoja wa mawinga hatari zaidi duniani.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England, aliye  umaliza msimu wa 2019/20 kwa kufunga mabao 20 na kutoa pasi 20 za mabao katika michuano yote.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *