Posted By Posted On

Bocco apewa somo kali

KOCHA wa zamani wa Simba, Abdallah Kibaden, amesema washambuliaji wa kigeni wa kikosi hicho, Middie  Kagere na Chris Mugalu wakiendelea na kasi ya kufunga mabao katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, nafasi ya John Bocco kucheza itakuwa ni finyu.

Akizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, Kibaden alisema uwezo ulioneshwa na washambuliaji hao unaweza kumsababishia Bocco kuendelea kusugua benchi kama hatamshawishi kocha wa timu hiyo  kujituma katika mazoezi.

“Usajili wa Simba msimu huu umelenga kuhitaji ushindi wa alama tatu pamoja na idadi kubwa ya mabao, hivyo lazima wawe na watu wa kuwatimizia hilo.

“Bocco ni mchezaji mzuri na mpiganaji, lakini si ana macho ya kuona mara kwa mara lango la wapinzani na hilo ndio tofauti yake na Mugalu na Kagere,” alisema Kibaden.

Kibaden ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Simba na Taifa Stars, alisema kama Mugalu na Kagere wakiendelea kuwa katika kiwango bora, Bocco  atasubiri  kwenye benchi la kikosi hicho.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *