Posted By Posted On

Cioaba, Dube wang’ara tuzo za Septemba

NA ZAINAB IDDY

KOCHA wa  Azam, Aristica Cioaba na mshambuliaji wake, Prince Dube, wameng’ara baada ya kutwaa tuzo ya ukocha na mchezaji bora wa Septemba wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Cioaba ametwaa tuzo hiyo, baada ya kuwashinda makocha wenzake alioingia katika fainali ya uchambuzi iliyofanyika wiki hii, Dar es Salaam na Kamati ya Tuzo ya Ligi unaopendekezwa na makocha  wanakuwa katika viwanja mbalimbali

Katika kinyang’anyiro hicho, Cioaba aliwashinda Sven Vandenbroeck wa Simba SC na Zlatko Krmpotic wa Yanga.

 Katika michezo ya Septemba ya ligi hiyo,  Cioaba alishinda michezo minne, wakati Sven na Zlatko kila mmoja alishinda michezo mitatu na sare moja.

 Tuzo ya mchezaji bora wa Septemba iliyokwenda kwa Dube kutokana na kuonesha kiwango kikubwa na kuiwezesha Azam kushinda michezo yote akiwa amefunga mabao mabao matatu huku Azam ikizoa pointi 12.

Katika kinyang’anyiro hicho Dube alikuwa akishindana na kipa wa Azam, David Kissu na kiungo wa Simba, Clatous Chama wote hawakupata kadi yoyote.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *