Posted By Posted On

Edu: Arsenal tuna njaa ya taji la EPL


LONDON, England

MKURUGENZI wa Ufundi wa Arsenal, Edu, amesema kuwa klabu hiyo ina ‘njaa’  ya taji la Ligi Kuu England (EPL) ambalo kwa mara ya mwisho, walilitwaa mwaka 2004.

Edu ametema cheche hizo ikiwa ni baada ya klabu yake hiyo kufanikiwa kumsajili kiungo hatari wa Atletico Madrid, Thomas Partey.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana, alijiunga na wakali hao wa London, siku ya mwisho wa kufungwa kwa dirisha la usajili wa kiangazi Jumatatu ya wiki hii, akitokea kwa wakali hao wa Hispania.

Partey mwenye umri wa miaka 27, ameungana na beki wa kati Gabriel Magalhaes, winga Willian, kiungo Dani Ceballos na kipa Runar Alex Runarsson waliojiunga na Washika Bunduki hao chini ya kocha Mikel Arteta.

Akizungumza na mtandao wa Arsenal, Edu alidai kuwa kikosi chake baada ya kumsajili Partey waliyemsotea kwa miezi kadhaa, kwa sasa wana njaa ya kuupigania ubingwa wa EPL. 

“Siku moja ningependa tuje kuwaonyesha mashabiki jinsi tunavyofanya kazi, au jinsi tulivyopambana kwa sababu ukiangalia mipango yangu ya miezi sita au saba iliyopita, niliyofanya na Mikel, tayari Thomas alikuwapo,” alisema Edu.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *