Posted By Posted On

Kagera ampotezea mpinzani wake

NA ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, raia wa Rwanda, Meddie Kagere, amemtaja mpinzani wake mkuu katika ufungaji wa mabao katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) ni Prince wa Azam, lakini hana mpango wa kumfikiria.

Dube aliyesajiliwa na Klabu ya Azam katika kipindi cha dirisha kubwa la usajili la msimu huu, tayari amefunga mabao matano katika michezo mitano ya ligi hiyo,huku Kagere akitupia mara nne.

Kagera ambaye ni mfungani bora katika misimu miwili ya Ligi Kuu Bara, hawezi kufikiria  anachofanya mshambuliaji mwenzake aliyeonekana kufunga kila mchezo wa ligi hiyo.

Akizungumza na BINGWA jijini Dar es Salaam jana, Kagere alisema jukumu lake ndani ya kikosi cha Simba ni kufunga na hana mpango wa kuangalia mwenzake anafanya anafanya kitu gani.

“Naona juhudi zake za kufunga na nikiri Dube ni mchezaji mzuri sana na anaonekana ana malengo makubwa sana , nampongeza kwa hilo kwa sababu mchezaji anayehitaji mafanikio lazima ajitume. “Lakini sioni sababu ya kumfikiria sana juu ya ufungaji wake wa mabao mara kwa mara, kila jambo linapangwa na Mungu ambaye ndiye ninamuamini kama msimu huu umepangwa niwe mfungaji bora kwa mara ya tatu nitakuwa tu, hivyo akili yangu itaendelea kuwaza jinsi gani naisaidia timu yangu.” Kagere

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *