Posted By Posted On

Keane, Wright wataka mashabiki waruhusiwe kuingia viwanjani

 

LONDON, England

WAKONGWE wa soka ambao kwa sasa ni wachambuzi wa mchezo huo, Ian Wright na Roy Keane, wameitaka serikali za mataifa ya Ulaya kuruhusu mashabiki kuingia

uwanjani. 

Timu ya Taifa ya England ilicheza mchezo wake wa kwanza nyumbani kwenye Uwanja wa Wembley dhidi ya Wales, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tangu kuibuka kwa janga la virus vya corona.

Katika mchezo huo wa juzi ambao England ilishinda mabao 3-0, timu hizo zilicheza huku viti vikiwa vitupu kutokana na hofu ya virus vya corona.

Akizungumzia kitendo hicho, mshambuliaji aliyewahi kutamba akiwa na Arsenal na England, Wright, alisema: “Ndiyo, nimevurugwa sana kuona ukubwa wa Wembley na jinsi mashabiki wanavyoweza kukaa kwa kupeana nafasi. 

“Watu wataogopa kuhusiana na janga hilo lakini unapoangalia hatua zinazochukuliwa, sielewi kwanini watu wasiruhusiwe kuingia.”

Kwa upande wake, Keane alisema kuwa timu ndogo zitaathirika mno kimapato kwani nyingi zinategemea fedha za viingilio.

“Klabu zitateseka sana, ukiangalia hali ilivyokuwa usiku wa leo (juzi), huwezi kuniambia kuwa watu 10,000 wasingeweza kuingia.” 

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *