Posted By Posted On

Kinda mwenye kipaji cha ajabu alia na majeraha

LONDON, England

WINGA wa Chelsea, Charly Musonda, ameelezea jinsi majeraha yaliyokatiza ndoto za kufanya makubwa katika soka.

Musonda aliyekuwa akitabiriwa kuwa mmoja wa makinda watakaotamba duniani kutokana na kuwa na kipaji cha kipekee, ameambiwa na daktari wake kuwa ana asilimia 20 tu ya kurejea kucheza soka kwa mara nyingine.

Kinda huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 23, alituma ujumbe huo kupitia katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram juzi Jumatano, uliowasikitisha wengi.

Akiwa na umri wa miaka 16, Musonda alielezewa kuwa kinda bora kabisa duniani, hivyo kunaswa na Chelsea mwaka 2012.

Hata hivyo, tangu mwaka 2016, Musonda, amekuwa nje ya uwanja kutokana na kukabiliwa na majeraha katika goti lake.

Musonda alisema: “Ni miaka minne imepita toka nilipocheza kwa mara ya mwisho mara kwa mara, baada ya hapo, majeraha yamekuwa yakinitesa na kushindwa kuonekana uwanjani.”

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *