Posted By Posted On

Majaliwa kuwashuhudia Stars

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ndiye atakuwa mgeni rasmi wa mechi ya kirafiki ya kimataifa, ambapo Taifa Stars kesho Jumapili Oktoba 11, 2020 itaikaribisha Burundi, Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Hassan Abbasi amethibitisha Majaliwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo ambao Stars, itakabiliana na Burundi.

Amesema mechi hiyo, imepangwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Dunia (FIFA), itawahusisha wachezaji wa Stars wanaocheza ndani na nje,watakaoongozwa na nahodha Mbwana Samatta.

"Kwasababu hiyo, tunawasisitiza Watanzania,kujitokeza uwanjani Jumapili saa 10:00 jioni kwa wingi kuishangilia timu yetu,ambayo itatumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi nyingine za kimataifa za kimashindano zitakazoanza Novemba mwaka huu," amesema  Abbasi na ameongeza kuwa.,Read More

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *