Posted By Posted On

Manula:Tumedhamiria kuitungua Burundi

NA MWANDISHI WETU

KIPA timu ya Tanzania, Taifa Stars, Aishi Manula, amesema wamejipanga kuibuka na ushindi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa  Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Manula alisema wanafahamu mchezo huo utakuwa mgumu, kwa kuwa wana kitu  ya ushindi watahitaji kupigana kwa jasho na damu ili waweze kutimiza malengo yao.

“Tutapambana kwa jasho na damu mbele ay Burundi, huu ni mchezo muhimu sana, ambao utatupa mwelekeo katika michuano inayokuja ya kimataifa.

“Tunawaomba mashabiki waje kutupa sapoti, huku wakiwa na imani na wachezaji kuwa tunaweza kuwapa ushindi wa mabao mengi Jumapili,” alisema Manula.

Kwa upande wake, Kocha msaidizi wa Taifa Stars, Seleman Matola, amesema wachezaji wao wapo katika viwango vizuri hivyo hawakuwa na kazi kubwa ya kutengeneza muunganiko.

“Wachezaji wamekuja kutoka katika klabu zao wakiwa na viwango vizuri, hii imetusaidia kutengeneza muunganiko kwa haraka ambao utatupa matokeo ya ushindi Jumapili (kesho),” alisema Matola.

Baada ya mchezo huo, Kikosi cha Stars  kitajiandaa na michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON ) kinachotajia kucheza na Tunisia Novemba 13, mwaka huu, ugenini  na kurudiana Novemba 17, nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *