Posted By Posted On

Mobetto kuzungumza na wajasiliamali Dar leo

NA JEREMIA ERNEST

MWANAMITINDO nyota na mfanyabiashara nchini, Hamisa Mobetto, ameweka wazi kuwa leo atakuwa na semina ya kuzungumza na wajasiliamali wadogo katika Chuo cha Utalii, Posta jijini Dar es Salaam.

Mobetto, ameliambia Papaso la Burudani kuwa kutakuwa na wakufunzi mbalimbali watakaozungumza na wajasiliamali lengo likiwa ni kutoa elimu ya kujiimarisha kwenye biashara zao.

“Nimeaanzisha utaratibu wa kutoa elimu kwa wajasiliamali wenzangu bila kujali unatembea mwendo mdogo kiasi gani kwenye biashara yako, hii ni semina ya siku moja na tutaanza na wajasiliamali 100,” alisema Mobetto.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *