Posted By Posted On

Shemeji Rotimi atua tuzo za Grammy

LOS ANGELES, MAREKANI

MWANAMUZIKI na mwigizaji staa wa Marekani ambaye pia ni mpenzi wa Vanessa Mdee, Olurotimi Akinosho a.k.a Rotimi, ametajwa kwenye orodha ya wasanii wanaofikiriwa kuingizwa kwenye vipengele vya tuzo kubwa duniani, Grammy 2021.

Rotimi mwenye asili ya Nigeria, ametajwa kufikiriwa kuingia kwenye vipengele vitatu ambavyo ni Best R&B Album (The Beauty of Becoming), Best R&B Song na Best R&B Performance kupitia wimbo wake, In My Bed.

Imekuwa kawaida kwa waandaaji wa tuzo za Grammy kutoa majina ya wasanii na watu mashuhuri ambayo hupitishwa kwenye mchujo na kupata majina yanayoingizwa kwenye vipengele 84 vya tuzo hizo.

,

Comments (0)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *